Posts

Showing posts from January, 2023

Kila Aliyefanikiwa Alifanya Uamuzi Huu Mkubwa.

Image
Katika maisha kila mmoja wetu anahitaji kufanikiwa. Lakini katika mafanikio kuna kanuni ambazo kila ambaye anahitaji kufanikiwa anapaswa kuzifahamu na kuzifanyia kazi. Na ndio maana katika maisha kuna watu waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa japokuwa wote wanawekeza juhudi kubwa kutafuta maisha. Hivyo kuna moja ambalo watu waliofanikiwa huwa wanalifanya na hivyo kuwatofautisha na watu wengine ambao hawafanikiwi. Katika Makala hii, tutaangalia jambo kubwa au uamuzi mkubwa ambao kila aliyefanikiwa alifanya. https://youtu.be/-N3kw7MYKMY?si=aMWnkeRzSmRLZjbv Tunapozungumzia mafanikio ni pana sana. Kwa mujibu wa Makala hii, mafanikio ni ile hali ya kufikia viwango ulivyojiwekea kwenye maisha yako. Viwango hivyo vinaweza kuwa: Kuwa na elimu kubwa, kuwa na biashara kubwa, Kuwa na kazi nzuri, Kukuza kipaji chako na kadharika. Hivyo katika Makala hii nitajikita kuelezea ni uamuzi gani mkubwa ambao kila aliyefanikiwa alifanya. Sasa, nianze na tabia ambayo watu wengi ambao ha...

Jambo Linalokuchelewesha Kufanikiwa.

Image
Mojawapo ya majuto ambayo watu wengi hupitia hasa umri wao unapokuwa umekwenda ni kuwa, hawakuishi maisha waliyokuwa wanayataka na kufanya kile kitu walichokuwa wanakipenda. Na pia hawakufikia malengo yao ya maisha kama walivyokuwa wanatamani kufikia. Katika Makala hii tutaangalia jambo kubwa ambalo limewachelewesha wengi kufanikiwa kufikia malengo yao ambalo pia linaweza kukufanya ushindwe kufanikiwa kwenye malengo yako na jinsi ya kukabiliana nalo. Tafiti nyingi sana zinaonesha watu wengi sana hasa wanapokaribia kufa hujilaumu maisha waliyoishi. Mwanasaikolojia mmoja anayeitwa Daniel Amend aligundua kanuni nzuri sana inayoitwa 18, 40, 60. Kanuni hii ilikuwa inasema hivi: Mtu anapokuwa na umri wa miaka 18-39 huwa anajiuliza nikifanya jambo hili, kazi hii au biashara hii watu watanionaje? Watu wa kundi hili maisha yote yanaendeshwa na maoni ya watu na sio utashi wao. Mtu huyu akifikisha umri wa miaka 40-59 huwa anaanza kusema, kwa sasa umri wangu umekwenda hivyo sitoj...

Jambo Moja La Kuzingatia Ili Uweze Kufanikiwa Katika Maisha.

Image
Karibu mpendwa msomaji katika Makala hii ya leo. Katika Makala hii nitaelezea jambo moja kubwa unalopaswa kulizingatia na kulifanyia kazi ili uweze kufanikiwa katika maisha. Inawezekana umekuwa ukitumia juhudi kubwa katika kazi zako ili uweze kujikwamua kimaisha lakini matokeo yanakuwa hayaonekani. Nikuhakikishie kuwa ukifuatilia Makala hii mwanzo hadi mwisho utakuwa umepata kitu cha msingi sana ambacho kitakusaidia uweze kufanikiwa katika maisha yako. Karibu tuendelee. Je ulishawahi kujiuliza ni kitu gani kinawatofautisha watu waliofanikiwa sana na wale ambao hawajafanikiwa? Katika Makala hii ya leo ningependa nikushirikishe kitu kimojawapo ambacho kinaweza kukusaidia sana kwenye maisha yako. Kitu hicho ni uwezo wa kupanga malengo na kuyafuatilia. Watu  wengi wanaamka kwenda kazini lakini ukiwauliza baada ya miaka kumi watakuwa akina nani hawawezi kukujibu. Sasa hebu nikushirikishe utafiti uliowahi kufanywa na Chuo Kikuu cha Havard cha nchini Marekani. Chuo kiku...