Tabia 8 Zinazozuia Fursa Za Mafanikio Maishani.
Katika Maisha, ili uweze kufanikiwa ni lazima uwe na uwezo wa kuchangamkia fursa zinazokuja mbele yako. Watu waliofanikiwa ni wale waliotumia kwa usahihi fursa ambazo walizipata. Ninapozungumzia fursa, ninamaanisha jambo lolote ambalo ukilipata litakufanya ufanikiwe Katika maisha. Mfano wa fursa ni kama vile kupata ajira, kupata mtaji wa biashara, kupata wateja kwenye biashara yako na kadhalika. Kimsingi, fursa hazitafutwi bali zinavutiwa. Kuna tabia ambazo mtu akiwa nazo zinamfanya aweze kuvutia fursa nyingi kwake. Lakini pia kuna tabia ambazo ukiwa nazo zinafukuza fursa. Unabaki unalalamika tu kuwa huna bahati ya mafanikio, kumbe mafanikio umeyazuia kutokana na tabia ulizonazo. Katika makala ya leo nitakushirikisha tabia nane zinazozuia fursa za Mafanikio kwenye maisha yako. Tabia 8 zinazozuia fursa za Mafanikio kwenye maisha yako. Mawazo hasi (negative thought) Mawazo hasi ni tabia inayoweza kuzuia fursa za Mafanikio. Mtu mwenye mawazo hasi ni mtu ambaye haamini kuwa anawe...