Jinsi Ya Kugundua Biashara Unayopaswa Kufanya Mtandaoni.
Katika somo lililopita la jinsi ya kupata wazo bora la biashara, nilielezea kanuni bora kabisa ya 7/7/7 ambayo ukiitumia inakuwezesha kupata mawazo mbalimbali mbalimbali ambayo yatakusaidia kuanzisha biashara yako ya mtandaoni. Kanuni hiyo ilikuwa na kazi ya kukupatia mawazo mbalimbali ambayo kupitia mawazo hayo uweze kupata wazo moja zuri ambalo utaanzishia biashara yako ya mtandaoni. K atika somo la leo tutaangalia Jinsi ya kugundua biashara unayopaswa kufanya (Discovering your niche). Jinsi ya kugundua biashara unayopaswa kufanya mtandaoni (Discovering your niche). Katika somo lililopita nilielezea kanuni ya 7/7/7 ambayo inakusaidia kupata mawazo mbalimbali ambayo yatakuwezesha kupata wazo moja la biashara. Katika kanuni hiyo, inakutaka kuorodhesha matatizo au changamoto 7 ambazo huwa unakabiliana nazo au watu wengine wanakabiliana nazo. Kisha unaorodhesha mambo 7 unayoyapenda (passions) halafu unamalizia na mambo 7 unayoyahofia( fears). Hivyo unakuwa umepata mambo 21 a...