Sifa 6 Chaneli Yako ya YouTube Lazima Iwe Nazo Ili Kufanikiwa
Tangu mwaka 2006, wakati Google iliponunua YouTube, jukwaa la video limeendelea kuwa maarufu. Leo hii, sio tu kwamba ni injini ya utafutaji ya pili kwa ukubwa baada ya Google, lakini pia ni tovuti ya tatu inayotembelewa zaidi mtandaoni. Hii imeleta fursa mpya na za kusisimua kwa wamiliki wa biashara ambao wanataka kuwafikia watazamaji na wateja wengi zaidi. Katika makala ya leo nitakushirikisha sifa 6 ambazo chaneli yako ya YouTube lazima iwe nazo ili uweze kufanikiwa. Sifa 6 Channel Yako ya YouTube Lazima Iwe Nazo Ili Uweze Kufanikiwa. 1.Kuwa na ratiba maalumu ya kuweka video. Channel ya YouTube yenye mafanikio zaidi , huweka video mpya kila siku au hata mara mbili kwa siku. Kwa aina hii ya kuweka video mara kwa mara, wafuasi wake daima huwa wanakumbushwa juu ya channel hiyo na wanapewa nafasi zaidi ya kuwasiliana na kampuni. Hivyo unahitajika kuwa na ratiba maalumu ya kuweka video mpya kwenye chaneli yako. Ikiwa hauna wakati wa kuandaa video kila siku, basi unahitajika k...