Tabia Kumi za Mafanikio Kutoka Kwa Watu Waliofanikiwa.
Mafanikio katika maisha yanatokana na tabia tulizozijenga na ambazo tunaishi nazo kila siku. Katika kusoma kwangu vitabu vya maendeleo binafsi (self development) niligundua kwamba ukiwasoma watu waliofanikiwa, unaanza kufundishwa misingi ya mafanikio. Ukiifuata misingi hii iliyothibitishwa ya mafanikio, na ukafanya kile ambacho wanaume na wanawake waliofanikiwa wamefanya katika historia, nawe pia utafanikiwa. Ugunduzi huu umenipa faida kubwa na ningependa kushiriki na wewe kuhusu baadhi ya misingi niliyogundua katika kusoma kwangu vitabu. Katika makala hii nitakushirikisha tabia kumi za mafanikio kutoka kwa watu waliofanikiwa. Tabia Kumi za Mafanikio Sifa hizi kumi ni tabia za kimaadili na hakuna mtu anayezaliwa nazo. Unaweza kujifunza na kuzikuza kwa kuzifanyia mazoezi. Ikiwa utazifanyia mazoezi hadi ziwe tabia yako, hakuna kitu kitakachokuzuia kufanikiwa . 1.Uwazi (Clarity) Sifa ya kwanza ni uwazi. Uwazi ni sehemu muhimu ya mafanikio. Inamaanisha kuwa na uwazi kw...