Jinsi Ya Kutumia Muda Vizuri: Parkinson Law
Kila mmoja amepewa masaa 24 katika siku moja. Lakini, jinsi tunavyotumia masaa tuliyopewa ndiyo itaashiria kiwango cha mafanikio yetu. Watu waliofanikiwa huwa wanatumia vizuri sana masaa ndani ya siku ili waweze kutimiza malengo yao na kufanikiwa katika maisha yao. Sasa, ni kwa jinsi gani watu waliofanikiwa hutumia muda wao? Wengi wao wanafahamu kanuni ya Parkinson na hivyo huwa wanatumia kupanga muda wao. Katika makala ya leo nitakushirikisha jinsi ya kutumia muda wako vizuri. Kanuni ya Parkinson inasema hivi: "Work expands to fill the time available for completion." Kwa lugha ya kiswahili ni kuwa, kazi huwa inachukua muda wote ulioutenga wa kuikamilisha . Hii ina maanisha kuwa, haijalishi ni muda mrefu kiasi gani ulioutenga kwa ajili ya kufanya kazi fulani, kwa muda ulioutenga, kazi yako itakamilika kwa muda huohuo. Kama umetenga muda mfupi, na kazi yako itakamilika ndani ya muda mfupi. Kwa mfano, kama umetenga dakika ishirini za kufanya kazi fulani, utatumia d...