Posts

Sababu 6 Usizozijua Zinazozuia Mafanikio Yako.

Image
Kila mmoja anahitaji kufanikiwa katika malengo aliyojipangia. Hata wewe ninaamini una malengo ambayo umeyaweka kwa mwaka huu Ili uweze kuyakamilisha. Malengo ambayo yatakutoa kutoka hatua moja kwenda nyingine. Watu wengi wamekuwa wakiweka malengo makubwa katika maisha yao lakini wameshindwa kupata matokeo waliyokusudia. Kuna sababu nyingi zinazochangia kushindwa kufikia malengo uliyojipangia. Katika makala ya leo nitakushirikisha sababu 6 usizozijua zinazozuia mafanikio kwenye malengo yako. Sababu 6 usizozijua zinazozuia mafanikio kwenye malengo yako. 1 . Kuwa na malengo mengi bila Kuweka vipaumbele. Miongoni mwa sababu zinazozuia mafanikio kwenye malengo yako, sababu ya kwanza kabisa ni kuwa na malengo mengi bila kuweka vipaumbele. Unapokuwa na malengo mengi, siyo rahisi kupata matokeo makubwa. Hii ni kwa sababu, kila lengo unaloliweka litahitaji rasilimali ya muda, nguvu, pesa na kadhalika. Kwa hivyo, unapokuwa na malengo mengi utajikuta kuwa unatawanya rasilimali za...

Jinsi Ya Kutumia Pesa Zako Vizuri Ili Ufanikiwe.

Image
Katika maisha kila mtu huwa anapata kipato. Kipato hiki inawezekana kikawa kinatokana na ajira, kujiajiri au kufanya biashara. Hata wewe ninaamini huwa unapata kipato. Lakini, mafanikio katika maisha, hayatokani na kiwango cha pesa unachopata bali yanatokana na kiwango unachobakiza kwenye kila pesa inayopita mkononi mwako. Hii ndio sababu unaweza kuona mtu fulani alikuwa anapata kipato kikubwa lakini baada ya muda unashangaa kuona kuwa amezidiwa maendeleo na mtu ambaye alikuwa na kipato kidogo. Hivyo, ili uweze kufanikiwa na kuwa na uhuru wa kifedha, ni lazima ufahamu Kanuni za fedha za kuzingatia. Katika makala ya leo nitakushirikisha jinsi ya kutumia pesa zako vizuri ili uweze kufanikiwa na kuwa na uhuru wa kifedha. Jinsi ya kutumia pesa zako vizuri ili uweze kufanikiwa. Katika makala hii nitakushirikisha kanuni moja ya fedha iliyotungwa na Northcoste Parkinson's. Kanuni hii inaitwa " Parkinson's law". Kanuni hii inasema: Siku zote matumizi ya mtu huwa yanaonge...

Jinsi Ya Kutumia Ujuzi Wako Kujiajiri Mtandaoni

Image
Katika maisha, kila mtu ana ujuzi wake. Ujuzi huu unatokana na kusomea chuoni, kufundishwa nyumbani au mtaani. Hata wewe inawezekana una ujuzi ambao umesomea chuoni au umejifunza mahali fulani. Changamoto kubwa ambayo inajitokeza hapa ni kwa jinsi gani unaweza kutumia ujuzi wako kujiajiri na kutengeneza kipato. Katika makala hii nitakushirikisha jinsi ya kujiajiri mtandaoni na kutengeneza kipato kwa kutumia ujuzi wako. Katika makala yangu ya njia 10 za kutengeneza pesa mtandaoni nilielezea kwa ufupi njia ambazo unaweza kuzitumia kuweza kujiajiri mtandaoni na kutengeneza kipato. Katika makala hii nitaelezea kwa kina njia moja ya kujiajiri mtandaoni ambayo ni kuanzisha blog. Hapa nitazungumzia jinsi unavyoweza kujiajiri kwa kuanzisha blog ya kitaalamu ( niche blog). Maana ya blog ya kitaalamu (niche blog). Niche blog au kwa Kiswahili blog ya kitaalamu ni aina ya blog ambayo imejikita katika kufundisha ujuzi wa aina moja. Hapa ina maanisha kuwa, kama wewe una maarifa au ujuzi wa kili...

Faida 10 Usizozijua Za Kuanzisha Blog Yako.

Image
Kwa nini unapaswa kuanzisha blog? Kama limekuwa ni swali ambalo umekuwa ukijiuliza kwa muda mrefu, basi nikuhakikishie kuwa, makala hii ni kwa ajili yako. Katika makala hii, nitakushirikisha faida 10 usizozifahamu za kuanzisha blog yako. Kabla ya kuendelea kwenye faida za kuanzisha blog, hebu kwanza nizungumzie maana ya blog pamoja na aina zake. Maana ya blog. Kwa tafsiri rahisi, blog ni aina ya tovuti. Aina hii ya tovuti inakuwa na vitu vifuatavyo: i. Makala : Blog inakuwa na makala ambazo zinaandikwa mara kwa mara. Kila makala moja inapoandikwa inakuwa juu ya makala ya zamani. Kwa mfano, kama uliandika makala juzi na jana, makala ya juzi itakuwa chini ya makala ya jana. Mfano mzuri wa blog ni hii uliyopo kwa sasa. ii. Sehemu ya kuweka maoni : Kila makala inapowekwa kwenye blog, kwa chini yake huwa kunakuwa na sehemu ya kuweka maoni. Hivyo, kama msomaji atakuwa amepata swali au maoni yoyote kuhusiana na makala husika, ataweza kuweka maoni yake kwenye sehemu ya kuwekea maoni. iii....

Mambo 3 Ya Kufanya Kila Siku Ili Kufanikiwa.

Image
Mafanikio Katika maisha yanategemea na jinsi unavyoitumia siku moja uliyopewa ya kuishi. Pia mafanikio ya siku yanategemea ni kwa namna gani umetumia vizuri masaa na dakika kwa siku hiyo. Kumbuka kuwa, muda ni rasilimali ya muhimu sana ambayo kila mtu amepewa kwa usawa. Hivyo, mafanikio yoyote Katika maisha yanategemea kwa kiwango kikubwa na jinsi unavyotumia muda wako. Kumbuka kuwa, haitoshi kuweka malengo ya mwaka, malengo hayo hayataweza kufanikiwa kama hautajua namna ya kuitumia vyema kila siku inayokuja na kupita. Maana ya mafanikio. Mafanikio ni neno pana sana na tafsiri yake inatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Kwa ujumla, mafanikio ni kuweza kufikia malengo uliyokusudia katika maisha yako kama vile: kuhitimu masomo, Kuanzisha biashara, kujenga nyumba, kuongeza kipato chako, kuwa na maisha mazuri na kadhalika. Hivyo, Kila mmoja anaweza kutafsiri neno mafanikio kwa kuhusianisha na malengo aliyojiwekea. Katika makala ya leo, nitakushirikisha mambo 3 muhimu ya kufanya ...

Kanuni Ya Kupata Mafanikio: “The Equal Odds Rule”

Image
Keith Simonton, mwanasaikolojia aliyehitimu masomo yake Chuo Kikuu cha Havard, mwaka 1977 alikuja na kanuni ya mafanikio inayojulikana kwa jina la The Equal Odds Rule. Kanuni hii aliiandika kwenye chapisho la “Creative productivity, age and stress: a biographical time-series analysis of 10 classical composers la mwaka 1977. Kanuni ya The Equal Odds Rule inasema hivi: “The average publication of any particular scientist does not have any statistically different chance of having more of an impact than any other scientist’s average publication.” Kwa tafsiri rahisi ni kuwa, chapisho lolote la mwanasayansi yoyote haliwezi kuleta matokeo makubwa na ya tofauti kuliko chapisho la mwanasayansi mwingine. Maana yake ni kuwa, ili mwanasayansi aweze kuleta matokeo makubwa na ya tofauti itategemea ni mara ngapi mwanasayansi huyo amerudia kufanya utafiti wa kile kitu kuliko wanasayansi wengine. Hivyo ndivyo kanuni hii ya The Equal Odds Rule inavyoelezea jinsi ya kupata mafanikio kwenye jambo ...

Kanuni Ya Mafanikio 'Choma Meli Zako Zote'

Image
Hernan Cortes, kamanda wa Hispania alikuja na Kanuni ya Mafanikio moja inayojulikana kama "Choma Meli Zako Zote'". Kanuni hii inatokana na kazi aliyopewa ya kwenda kuvamia kisiwa kilichokuwa kinajulikana Kwa jina la Veracruz nchini Mexico mwaka 1519. Kitu alichokifanya ni kuwa, alichukua makamanda 500 pamoja na Meli 11 za kivita na akawapandisha kwenda kuvamia kwenye kile kisiwa. Alipofika kwenye kile kisiwa, akaamuru makamanda pamoja na mabaharia wote washuke. Baada ya wote kuwa wameshuka, akaagiza Meli Zote zichomwe moto. Wakati Meli zilipokuwa zinaungua, akawauliza makamanda pamoja na mabaharia " mnaona nini?" wakamjibu "Tunaona moto pamoja na moshi, meli zetu zinaungua". Akawaambia " Hivyo basi, hatuna uchaguzi zaidi kwenye vita hii. Ni lazima tuchague moja kati ya mambo haya mawili: Moja, tuamue kufa tushindwe vita, au pili, tupigane tushinde vita ambayo tumeianza." Unajua nini kilitokea? Ingawa walikuwa ni wachache ukil...