Posts

Jinsi Ya Kugundua Biashara Unayopaswa Kufanya Mtandaoni.

Image
Katika somo lililopita la jinsi ya kupata wazo bora la biashara, nilielezea kanuni bora kabisa ya 7/7/7 ambayo ukiitumia inakuwezesha kupata mawazo mbalimbali mbalimbali ambayo yatakusaidia kuanzisha biashara yako ya mtandaoni. Kanuni hiyo ilikuwa na kazi ya kukupatia mawazo mbalimbali ambayo kupitia mawazo hayo uweze kupata wazo moja zuri ambalo utaanzishia biashara yako ya mtandaoni. K atika somo la leo tutaangalia Jinsi ya kugundua biashara unayopaswa kufanya (Discovering your niche). Jinsi ya kugundua biashara unayopaswa kufanya mtandaoni (Discovering your niche). Katika somo lililopita nilielezea kanuni ya 7/7/7 ambayo inakusaidia kupata mawazo mbalimbali ambayo yatakuwezesha kupata wazo moja la biashara. Katika kanuni hiyo, inakutaka kuorodhesha matatizo au changamoto 7 ambazo huwa unakabiliana nazo au watu wengine wanakabiliana nazo. Kisha unaorodhesha mambo 7 unayoyapenda (passions) halafu unamalizia na mambo 7 unayoyahofia( fears). Hivyo unakuwa umepata mambo 21 a...

3. Jinsi Ya Kutafuta Wazo La Biashara Yako Ya Mtandaoni.

Image
Ikiwa wewe ni kama watu wengine wanaotarajia kumiliki biashara mtandaoni, unaweza kuwa na mawazo mengi sana ya aina ya biashara unazotaka kuanzisha au inawezekana ukawa hauna wazo lolote. Vyovyote vile iwavyo, somo hili litakusaidia jinsi ya kutafuta wazo bora la biashara yako ya mtandaoni. Tutaangalia jinsi ya kupata wazo bora kwa kutumia zoezi rahisi la 7/7/7. Jinsi ya kupata wazo bora la biashara yako ya mtandaoni kwa kutumia zoezi rahisi la 7/7/7. Katika somo hili tutafanya zoezi rahisi na la kufurahisha sana ambalo litakusaidia kugundua wazo la kuchagua kwenye biashara yako unayotarajia kuanzisha mtandaoni. Zoezi hili litakusaidia sana kama haujui mahali pa kuanzia kupata wazo bora la biashara yako. Lakini pia hata kama una rundo la mawazo kichwani kwako, zoezi hili litakusaidia kukupunguzia mawazo hayo na hivyo kubaki na mawazo machache ambayo utayafanyia kazi. Sasa, zoezi hili linaitwa zoezi la 7/7/7. Madhumuni halisi ya zoezi hili ni kuangalia matatizo saba, m...

2. Biashara Inayolipa Mtandaoni Ni Ipi?

Image
Kabla ya kujenga biashara yenye mafanikio, jambo la kwanza kabisa tunapaswa kwanza kuelewa ni nini kinafanya biashara kufanikiwa. Katika somo la hili la pili nitakushirikisha jinsi ya kutambua Biashara inayolipa mtandaoni. Somo hili litaweka msingi wa masomo yangu mengine yanayofuata katika mfululizo wa masomo haya ya Jinsi ya kuanzisha biashara mtandaoni. Biashara inayolipa mtandaoni na yenye mafanikio ni ipi? Kuna biashara za aina nyingi mtandaoni na nje ya mtandao. Kuna nyingine zimefanikiwa na nyingine hazijafanikiwa. Hivyo, kabla ya kuanzisha biashara yoyote mtandaoni ni lazima utambue ni biashara gani itakulipa na kukuletea mafanikio. Kimsingi, biashara inayolipa na yenye mafanikio sana ni biashara ambayo imejikita katika kutatua tatizo fulani katika jamii. Hivyo, biashara zote zilizofanikiwa hutatua matatizo au changamoto zilizopo katika jamii. Katika somo linalofuata ambapo tutaangalia Jinsi ya kutafuta wazo bora la biashara yako ya mtandaoni, nataka na wew...

Jinsi Ya Kuanzisha Biashara Mtandaoni: 1. Utangulizi.

Image
Karibu mpendwa msomaji wangu katika mfululizo wa masomo haya ya Jinsi ya kuanzisha biashara mtandaoni. Katika masomo haya ambayo yanaanza leo, nitaelezea hatua kwa hatua jinsi ambavyo unaweza kuanzisha biashara yako mtandaoni na ukatengeneza kipato. Katika masomo haya nitaelezea mambo mengi yakiwemo: Jinsi ya kuchagua wazo la biashara yako. Hii itakuwa ni sehemu ya kwanza kabisa. Na kisha nitaelezea jinsi ya kupima soko la biashara yako na hivyo kuwa na uwezekano wa kuuza. Kuangalia soko kwa ujumla itakusaidia kupata uelewa wa jinsi utakavyoingia katika soko la mtandaoni ukiwa na kitu cha kipekee na hivyo kukufanya ujulikane na kuliteka soko. Katika masomo haya tarajia kufanya mazoezi machache ili kufahamu wazo bora la biashara yako, hii ni kwa sababu, mara nyingi tunaweza kuwa na mawazo mengi ya biashara yanayopita kwenye vichwa vyetu. Hivyo nitaelezea jinsi ya kuchagua wazo moja sahihi la biashara yako. Pia inawezekana ukawa hauna wazo la biashara hata moja, nitaku...

Jinsi Ya Kuwa Na Mafanikio Maishani: Tabia 15 Za Kuzingatia

Image
Iwe unaamini au la kwa wakati huu, tambua ya kuwa una uwezo wa kufanya mambo makubwa na ya ajabu katika maisha yako. Mara nyingi, tunachohitaji ili kufanikiwa maishani na kutenda kulingana na uwezo mkubwa tulionao ni kujua tu jinsi ya kuanza, kubaki thabiti katika malengo yetu na kufuata hatua sahihi ili kufikia mafanikio yetu. Hivyo, kwa kufuata mazoea fulani muhimu, utaweza kufanikiwa maishani. Iwe ni katika maisha yako binafsi au kazini, hakuna atakayeweza kuzuia mafanikio yako. Katika makala ya leo nitakushirikisha jinsi ya kuwa na mafanikio makubwa katika maisha. Nitaelezea kwa kina tabia 15 ambazo unapaswa kuwa nazo ili uweze kufikia mafanikio makubwa katika maisha yako. Jinsi ya kufafanua maana ya mafanikio. Kila mtu huwa na wazo tofauti la jinsi mafanikio yanavyoonekana au yanavyopaswa kuwa kwake. Kwa hiyo, kufafanua na kupima mafanikio lazima kufanyike kwa mtu binafsi. Kwa mfano kwako, je, mafanikio kwako yanamaanisha mafanikio ya kifedha? Mafanikio ya ki...

Dondoo Za Namna Ya Kununua Na Kuuza Mtandaoni.

Image
Fahamu maana ya biashara ya kununua na kuuza mtandaoni (E-Commerce). Je, umekuwa ukijiuliza nini maana halisi ya kufanya biashara na kupata kipato kupitia intanet? Au pengine ulikuwa ukijiuliza maswali mengi kuwa unaanzaje kuuza au kununua kwenye intaneti ? Hapa utajifunza na kufahamu maana halisi ya ecommerce na jinsi inavyofanya kazi. Mwisho wa siku utakuwa muuzaji au mnunuaji kupitia intaneti. Na kwa maana hiyo utakuwa miongoni mwa mamilioni ya watu ambao wamekamata fursa za kibiashara kutumia intaneti. Maana ya Ecommerce. Maana ya ecommerce ni kitendo cha kuuza au kununua bidhaa na/au huduma kwa njia ya intaneti. Shughuli hii haijaanza leo bali ilianza miaka ya 1960 baada ya kuibuka teknolojia iitwayo Electronic Data Interchange (EDI) ambapo mfumo huo uliwezesha makampuni au watu kuweza kubadilishana hati, hundi au risiti za kibiashara kwa kutumia komputa zilizounganishwa na intaneti. Shughuli hiyo ilishika kasi zaidi kufikia miaka ya 1990 na mwanzo wa 2000. Mfano mw...

Jinsi ya Kuweka Malengo ya Kifedha na Kuyafikia kwa Ufanisi

Image
Malengo ya kifedha ni mipango au ndoto unazotaka kuzitimiza kwa kutumia pesa zako. Kwa mfano, unaweza kuwa na lengo la kununua nyumba, kusomesha watoto, kustaafu kwa amani, au kusafiri duniani. Malengo haya yanaweza kuwa ya muda mfupi, wa kati, au mrefu, kulingana na muda unaohitajika kuyafikia. Kuweka malengo ya kifedha ni hatua muhimu katika kujenga msingi imara wa kifedha na kuishi maisha bora. Malengo ya kifedha hukusaidia kujua unachotaka kufanya na pesa zako, kupanga bajeti yako, kuweka akiba, kuwekeza, na kudhibiti matumizi yako. Malengo ya kifedha pia hukupa motisha, mwelekeo, na kipimo cha maendeleo yako. Hata hivyo, kuweka malengo ya kifedha peke yake haitoshi. Unahitaji pia kuchukua hatua za kuyafikia malengo hayo kwa ufanisi. Hii inahitaji nidhamu, uvumilivu, na ufuatiliaji wa mara kwa mara. Vinginevyo, malengo yako yatakuwa tu ndoto zisizotimia. Katika makala hii nitakushirikisha hatua nne za kufuata ili uweze kuweka malengo ya kifedha na kuyafikia kwa ufanisi...